CHADEMA Yapinga Wawekezaji Kunyang'anywa Viwanda Walivyobinafsishiwa


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Serikali haiwezi kujenga viwanda peke yake bila kuihusisha sekta binafsi ambayo ndiyo mdau mkuu katika uwekezaji nchini.

Mbowe amepinga kusudio la Rais John Magufuli kuwanyang'anya wawekezaji viwanda walivyobinafsishiwa kwa madai kwamba Serikali ilitakiwa kutafuta chanzo cha kufungwa kwa viwanda hivyo kabla ya kufikia uamuzi wake.

Mwenyekiti huyo amebainisha sababu mbalimbali zilizofanya viwanda hivyo visifanye kazi kuwa ni pamoja na kutopatiwa ruzuku na Serikali, teknolojia ya zamani ya viwanda hivyo na wakati viwanda hivyo vinajengwa kulikuwa na mfumo hodhi wa soko.

"Hakuna mfanyabiashara duniani àmbaye atapewa kitega uchumi kinachozalisha halafu akakifunga. Hayupo!" amesema Mbowe.

Amesema Rais Magufuli hana mapenzi na sekta binafsi kwa kuwa anaamini kwamba kila mtu aliye kwenye sekta binafsi ni "mpiga dili."

"Viwanda vingi vimefungwa kwa sababu ya kodi mbaya hazilipiki, gharama ya kufanya biashara Tanzania ni maumivu makubwa sana.

"Takwimu za benki kuu zinasema kuwa kwenye benki za biashara Viwanda vimekopa 0%

"Viwanda vingi vilishindwa kuendeshwa kwa sababu vingi vilikuwa na teknolojia ya zamani"  Amesema Mbowe

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment