Chelsea wamefikia makubaliano kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata kwa ada inayoripotiwa kuwa £70m.
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uhispania sasa anatakiwa kuafikiana masuala yake ya kibinafsi na klabu hiyo na pia achunguzwe hali yake ya kiafya kabla ya kukamilisha uhamisho wake.
Morata, 24, atakuwa mchezaji wa nne kununuliwa na mabingwa hao wa Ligi ya Premia majira haya ya joto, baada ya kipa Willy Caballero, beki Antonio Rudiger na kiungo wa kati Tiemoue Bakayoko.
Morata alifunga mabao 20 msimu uliopita baada ya kujiunga na Real kutoka Juventus.
Morata alifunga mabao 20 msimu uliopita baada ya kujiunga na Real kutoka Juventus.
Alishinda taji la La Liga na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu uliopita, lakini mara nyingi alikuwa akicheza kama nguvu mpya.
Morata huenda akachukua nafasi ya mwenzake wa Uhispania Diego Costa, ambaye anasema aliambiwa na meneja wa Chelsea Antonio Conte kwamba hayupo tena katika mipango ya klabu hiyo. Manchester United walikuwa wakitaka kumnunua Morata kabla ya kumnunua mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku kwa £75m. Morata alijiunga na timu ya wachezaji chipukizi Real Madrid mwaka 2008 na akachezeshwa timu kubwa akiwa na miaka 18 mwaka 2010.


0 comments :
Post a Comment