HASIRA HASARA:Aua mkewe baada ya kuchekwa sana na mkewe huyo

Mwanaume mmoja nchini Marekani anatuhumiwa kumuua mke wake kwa sababu mke huyo alikuwa akimcheka sana yeye, wanasema polisi.
Mwanaume huyo Kenneth Manzanares kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi na alikamatwa baada ya kukutwa na damu mikononi na kwenye nguo zake.
Tukio hilo limetokea Jumanne hii jini Alaska wakati wanandoa hao walipokuwa kwenye meli ya starehe ambapo mwili wa mwanamke huyo Kristy Manzanares(39) ukikutwa katika moja ya vyumba vya meli hiyo.
Mmoja wa mashuhuda ambaye aliingia kwenye chumba cha meli walimokuwemo wanandoa hao anasema alimuona mtuhumiwa akiuburuta mwili wa mwanamke huyo kuupeleka sehemu ya nje ya kupumzikia kwenye meli hiyo.
Hali hiyo ikamfanya shuhuda huyo kuukamata mkono wa mwanamke huyo nakumvuta kumrejesha ndani ya meli.
Shuhuda huyo anasema, alipomuuliza mtuhumiwa nini kimetokea, mtuhumiwa huyo alisema: “Mwanamke huyu alikuwa haachi kunicheka.”
Mtuhumiwa huyo anatajia kumfikishwa mahakamani Agosti 10 mwaka huu
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment