Kwa sasa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania yuko ziarani mkoani mwanza hii ni kanda ya ziwa
Hapo awali baada tu ya kuapishwa mheshimiwa rais amekuwa na mfululizo wa ziara nyingi mikoa ya kanda ya ziwa, hii inanipa wasiwasi na kunipa maswali kadhaa
Kuna nini cha muno huko kanda ya ziwa kisichopatikana mkoani Kwangu Rukwa?, mbeya, iringa tabora na kigoma?
Inamaana yeye ni rais wa kanda ya ziwa tu kila uchwao utamskia karudi chato!
Rais wangu nikwambie tu, Tanzania ni zaidi ya kanda ya ziwa
Umeshindwa kutoka nje ya nchi, yaani hata mikoa ya nchi yako pia imekushinda!?
Rais wa Tanzania umerudi mwanza kiziara zaidi ya mara tatu sasa ilihali kuna mikoa huijui kabisa tangu upewe kura zao, hata shukrani hukuwai toa!
Tanzania ni zaidi ya Chato rais wangu! Toka huko zunguka nchi nzima na izo unazodai ni ziara
SOURCE:JF
0 comments :
Post a Comment