JPM:Wanaompinga kafulila ni matumbili.


Rais wa Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amempongeza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila kutokana na namna alivyojitoa katika kutetea maslahi ya Watanzania kwenye sakata la Escrow(IPTL) na kuonesha uzalendo mkubwa ambao hawezi kusahaulika katika historia ya Tanzania.
Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Nguruka katika hafla ya uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza ambapo alisema kuwa akiondoka hapo bila kumpongeza Kafulila atakuwa amefanya dhambi ya unafiki itakayompeleka motoni.
Akizungumza, Rais alisema anatambua kwamba Kafulila yupo chama kingine, lakini kwenye suala la IPTL, aliweka maslahi ya Taifa mbele na kusimamia ukweli hivyo anampongeza na pongezi hizo ni za dhati kwani zinatoka moyo. Rais alieleza umma uliokuwa umejitokeza mahali hapo kuwa, wizi uliokuwa unafanywa na IPTL ni mkubwa hivyo Kafulila alisimama kutetea umma wa watannzani.
Lakini pia Rais alieleza vikazwo ambavyo Kafuli alikutana navyo wakati akipambana kuhusu wizi huo uliokuwa ukiratibiwa na baadhi ya watumishi wa serikali kwa manufaa yao wenyewe.
“Wakamtisha wengine kumpeleka mahakamani, wakamtukana wee, wengine wakamuita tumbili, sasa tumbili amefanya makubwa kwa ajili ya Watanzania. Wao ndio matumbili, huyu (Kafulila) alifanya kazi ya Mungu ya kuwatumikia Watanzana,” alisema Rais Magufuli huku wakazi wa eneo hilo wakilipuka kwa furaha.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment