Lipumba amwita Seif Buguruni

  • Profesa Lipumba amesema yeye ni mwenyekiti halali wa CUF na amemtaka katibu wake Maalim Seif arejee ofisini kuendelea na majukumu yake ambayo kwa sasa yanakaimiwa na Magdalena Sakaya.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad ameshindwa kutekeleza majukumu yake kama kiongozi.
Hata hivyo, Profesa Lipumba amemtaka arejee ofisini kuendelea na majukumu yake licha ya kudai kwamba kwa sasa nafasi yake inakaimiwa na Naibu Katibu Mkuu, Magdalena Sakaya.
Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni leo, Profesa Lipumba amesema bado anamtambua Maalim Seif kama Katibu Mkuu wa chama hicho licha ya utoro wake kazini.
"Sijamwona Katibu Mkuu tangu Septemba 23 mwaka jana, namkaribisha aje ofisini Buguruni apokee maelekezo kutoka kwa mwenyekiti," amesema Profesa Lipumba.
Mwenyekiti huyo amesisitiza kwamba yeye ni mwenyekiti halali wa CUF kwa mujibu wa ibara ya 117 ya chama hicho ambayo inaeleza taratibu za kiongozi kujiuzulu.
"Ibara ya 117 inatoa mamlaka kwa mkutano mkuu kujadili barua ya kiongozi kisha kuridhia kujiuzulu kwake au laa. Sasa mimi niliandika barua ya kutengua kujiuzulu kwangu kabla mkutano mkuu wa chama haujakaa kuijadili barua yangu ya kujiuzulu," amesema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment