- ACT imemtaka Waziri Tizeba ajiuzulu kutokana na usumbufu wanaoupata wakulima wa korosho ambao umesababishwa na ahadi hewa ya Serikali ambayo inaweza kusababisha uzalishaji wa korosho kushuka.
Chama cha ACT-Wazalendo kimemtaka Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba kujiuzulu kwa kushindwa kuwapelekea wakulima wa korosho pembejeo kama alivyoahidi.
Serikali iliahidi kuwapa wakulima wa korosho dawa ya kuua wadudu sulpher bure ili waongeze uzalishaji.
Akizungumza leo Jumapili, Katibu wa Itikadi,Mawasiliano ya Umma na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu amesema kwa sasa kuna upungufu wa pambejeo hiyo.
Amesema Serikali iliahidi kupeleka tani 5000 za sulphur lakini imepeleka tani 1500 tu. Amesema matokeo yake, wafanyabiashara wanauza sulphur hadi kufikia Sh80,000 kwa mfuko mmoja badala ya Sh30,000.
0 comments :
Post a Comment