Madiwani watatu wa Jimbo la HAI ,Kilimanjaro watangaza kujiunga na CCM wakitokea CHADEMA

Wimbi la Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kujiunga na Chama
cha Mpinduzi (CCM) likiwa limepamba moto mkoani Arusha, majirani zao wa Kilimanjaro nao wameanza kutimka kwa kile wanachodai kuwa ni kuweza kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe
Magufuli.
Mapema leo mchana Julai 26, 2017, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole
amewapokea madiwani watatu kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai ambao wametangaza
kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga CCM.
Madiwani waliojiuzulu ni, Diwani wa Kata ya Machame Magharibi, Goodluck Kimaro, Diwani wa
Kata ya Weruweru, na Diwani wa Kata ya Mnadani, Everist Peter Kimati.
Akizungumza wakati wa kutangaza azma hiyo, Goodluck Kimaro alisema kwamba CHADEMA
hakuna demokrasia kama ambavyo chama hicho kimekuwa kikijinasibu. Akitolea mfano Halimashauri ya Wilaya ya Hai ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ni Mbunge wa jimbo hilo, alisema chama hakina uwezo wa kufanya jambo lolote dhidi ya mbunge.
Endapo mbunge atashindwa kutekeleza majukumu yake, chama ndio kinatakiwa kumuadhibu,
lakini kwa upande wetu wa Hai hakuna uongozi wa kuweza kufanya hivyo. Mbunge huwa hafanyi
ziara za kutembelea jimbo kama anavyotakiwa, lakini bado chama hakina sauti, alisema Goodluck
Kimaro.
Baada ya madiwani wote kuzungumza, Polepole alionya juu ya uwepo wa vitendo vya kihalifu kwa madiwani ambapo wanahama CHADEMA na kusema jambo lolote likitokea kwa madiwani hao, watashughulikiwa ipasavyo na vyombo vya dola lakini pia chama hicho kingine ndio watakuwa
wahusika.
Hadi sasa jumla ya madiwani 9 mkoani Arusha tayari wamejiunga na CCM na sasa watatu mkoani
Kilimanjaro nao wamejiunga.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment