Majaliwa aagiza kukamatwa wahusika hasara bilioni 63 Mbeya

Waziri mkuu Kassim Majaliwa, leo Julai 31, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kuwakamata waliolisababishia Jiji la Mbeya hasara ya kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 63.
Kwa mujibu wa mwandishi wa Azam TV ,Kakuru Msim aliyepo mkoani Mbeya, wahusika hao ambao miongoni mwao bado wapo madarakani ni pamoja watu watatu waliowahi kuwa wakurugenzi wa jiji hilo na makaimu wakurugenzi wawili.
Katika sekeseke hilo ambalo limeibuliwa na waziri mkuu Majaliwa, yupo pia kaimu mweka hazina na meya mstaafu Athanas Kapunga.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa, yupo mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi ya siku tano
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment