Majadiliano kati ya kamati maalum iliyoundwa na rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli na wawakilishi kutoka Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo nchini yameanza leo tarehe 31 Julai, 2017 jijini Dar es Salaam.
Kamati maalum ya Tanzania inaongozwa na waziri wa sheria na katiba, Prof. Palamagamba Kabudi na kamati ya kutoka Barrick Gold Corporation inaongozwa na afisa mwendeshaji mkuu Richard Williams.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa majadiliano hayo Prof. Kabudi amesema kamati yake imejipanga vizuri kujadiliana na Barrick Gold Corporation juu ya madai ya Tanzania katika biashara ya madini ya kampuni hiyo nchini na itahakikisha inasimamia maslahi ya Tanzania ipasavyo.
Kwa upande wake, Richard Williams ameshukuru kuwepo kwa majadiliano hayo na amesema kampuni ya Barrick Gold Corporation imeyapokea madai ya Tanzania kwa mtazamo chanya na ipo tayari kujadiliana na kufikia makubaliano yenye maslahi kwa pande zote mbili.
0 comments :
Post a Comment