Tetemeko dogo la ardhi latokea Karagwe

  • Tetemeko kubwa la ardhi lilitokea Septemba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 16, nyumba 840 kuanguka na nyingine 1,264 kupata ufa.
Tetemeko lililodumu kwa takriban sekunde tano limetokea leo, Julai 30 saa nne asubuhi katika  Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kayanga wilayani Karagwe, lakini hakuna madhara yaliyoripotiwa  kutokea.
Ofisa wa Wakala wa  Jiolojia Tanzania, Gabriel Mbogani amesema ili kupata uhakika wa tetemeko hilo ni lazima kukusanya taarifa kwenye mitambo.
Amesema wananchi mkoani Kagera kwa sasa wapo makini  baada ya kupatiwa semina kutokana na tetemeko la Septemba mwaka jana ambalo lilisababisha madhara makubwa.
“Wananchi wa Bukoba baada ya semina tulizotoa  na kuwaonyesha ramani ya matukio ya tetemeko  wamekuwa na uelewa, hivyo hata likitokea dogo  kiasi gani lazima watoe taarifa,” alisema Mbogani.
Hata hivyo, amewataka wananchi kuendelea  kuchukua tahadhari kwa kuwa haijulikani ni muda  gani tetemeko kubwa linaweza kutokea kwa kuwa uzoefu ni kuwa huanza dogo na baadaye kuwa kubwa.
Mkazi wa mji mdogo wa Kayanga, Elieth Kikaka  amesema alitoka nje ya nyumba baada ya tetemeko hilo kwa kuwa yamekuwa yakitokea mara kwa mara mkoani Kagera hivyo linapotokea ni lazima  kuchukua tahadhari.
Mwisho
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment