DC aagiza wauguzi kufukuzwa kazi


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dodoma, Deogratius Ndejembi, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwachukulia hatua za kisheria ikiwamo kuwafuta kazi wauguzi 4 wa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa kufanya uzembe na kusababisha kifo cha mtoto mchanga
Bw. Ndejembi ametoa agizo hilo baada ya kupokea ripoti ya kamati aliyoiunda kuchunguza sakata la madai ya wauguzi hao kusababisha kifo cha mtoto mchanga kwa uzembe Juni 29 mwaka huu pamoja na madhara ya kiafya kwa mama wa kichanga hicho ambaye pia tukio hilo limemuathiri kisaikolojia.
Awali kabla ya Mkuu huyo wa Wilaya kutoa maagizo Katibu wa Kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo Celina Fundi aliwasilisha ripoti ya uchunguzi wa kamati uliobaini kwamba, wauguzi hao walihusika kwa namna moja kwa kufanya uzembe na kutoa mapendekezo yake.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dk. Magareth Kagashi amewakumbusha watumishi wa idara ya afya kutambua kuwa huduma bora kwa wagonjwa ni wajibu wao kwani wamekula kiapo kuwatumikia wananchi na si vinginevyo.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment