Mbunge wa CHADEMA akamatwa na Polisi

Songwe, Pascal Haonga, amekamatwa na Polisi leo mchana katika mji mdogo wa Mlowo­Mbozi.
Mbunge huyo anahojiwa na polisi na sababu za kukamatwa kwake bado hazijafahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange, amethibitisha kumshikilia Haonga lakini hakutaka kueleza suala hilo kwa kina kwa madai yupo nje ya ofisi.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Songwe, Meshack Mgaya amesema wanaendelea kufuatilia kwa ukaribu juu ya tukio hilo na baadae chama kitatoa tamko baada ya kujiridhisha sababu za kukamatwa kwa Mbunge huyo.
Chanzo cha habari:Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment