Mbunge wa Kawe na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi wa kambi ya upinzani bungeni, Halima Mdee ameijibu taarifa iliyotolewa na msemaji wa serikali Dkt.Hassan Abbasi kwa kuikosoa na kudai haina ukweli kwamba uchumi wa nchi umekuwa imara kwa miaka mitatu mfululizo.
Mdee ameeleza hayo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya kuwepo kwa taarifa iliyotolewa Agosti Mosi mwaka huu kutoka kwa Dkt. Abbasi inayosema takwimu za Benki Kuu (BoT) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) zimetaja uchumi wa Tanzania kuwa bado uko imara kwa miaka mitatu mfululizo katika ukuaji usiyopungua asilimia 7.0 hadi 7.2.
“Uchumi wetu ulianza kukuwa kwa asilimia 7 tokea temu ya pili ya Rais Mkapa ambayo ni mapinduzi ya kiuchumi ya kipindi hicho. Kwa hiyo ni kweli uchumi umekuwa kwa asilimia 7 tena siyo miaka mitatu, mwaka 2011 ulikuwa zaidi ya asilimia 7.9 sasa majibu ambayo tunayataka watuambie huu uchumi ambao haukui, umekuwa pale pale miaka yote umeweza kuwa ‘reflected’ vipi kwa maisha ya Mtanzania wa kawaida hayo ndiyo majibu tunayoyataka”, amesema Mdee.
Pamoja na hayo Mdee ameendelea kwa kusema “sisi tuitake serikali watuambie ni kwa kiwango gani uchumi wa nchi umekuwa. Kwa maana hii asilimia saba tunayoijua haijaanza kwa Jakaya ilianza kwa Mkapa ikaja kwa Jakaya na huyu Mhe. Magufuli amekutana nayo kwa hiyo watuambie imekuwa ‘reflected’ vipi kwa maisha ya kawaida kwa Mtanzania, mkulima na mfanyakazi” . amesema Halima Mdee
Kwa upande mwingine, Mdee ameitaka serikali ieleze ni kwa nini sekta ya kilimo imeporomoka na itoe mpango mkakati wa kuinua kilimo nchini.
Kwa upande mwingine, Mdee ameitaka serikali ieleze ni kwa nini sekta ya kilimo imeporomoka na itoe mpango mkakati wa kuinua kilimo nchini.
0 comments :
Post a Comment