Victor Hangaya alipata umaarufu msimu uliopita baada ya kuwatungua klabu ya Simba magoli mawili peke yake kwenye ushindi wa goli mbili kwa moja.
Klabu ya Mbeya City imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Victor Hangaya kwa mkataba wa miaka miwili.
Kupitia akaunti yao maalumu ya instagram, kaimu Afisa Habari wa Mbeya City Shah Mjanja, amethibitisha kumalizana na Hangaya kwa mkataba wa miezi 24 kwa kuposti picha ikimuonesha mshambuliaji huyo akiwa na jezi ya Mbeya City.
“Mapema leo hii klabu yetu imekamilisha usajili wa mshambuliaji Victor Hangaya na kukabidhiwa jezi nambari 27. Hangaya ambaye anajiunga na City kwa kandarasi ya miezi 24 amefurahi sana kujiunga na kikosi chetu cha maangamizi kilichorejea hivi karibuni kutoka katika mashindano huko Morogoro.
Kila la kheri Hangaya.” ameandika hivyo kaimu Afisa Habari huyo
Kila la kheri Hangaya.” ameandika hivyo kaimu Afisa Habari huyo
Victor Hangaya alipata umaarufu msimu uliopita baada ya kuwatungua klabu ya Simba magoli mawili peke yake kwenye ushindi wa goli mbili kwa moja, mchezo uliopigwa kwenye dimba la Sokoine mwaka jana.
Mbali na Victor Hangaya kadhalika Prisons imempoteza pia, Mohhamed Samatta aliye saini Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea kwa maafande hao wa jijini Mbeya.
0 comments :
Post a Comment