imba kuwasili Dar kesho tayari kuanza msimu mpya VPL

Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kurejea nchini kesho mchana baada ya kambi ya takriban wiki mbili nchini Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.
Simba inatarajiwa kuwasili nchini kwa makundi mawili, kundi la kwanza likifika Saa 7:00 mchana na kundi la pili kuingia saa 7:00 Usiku kutokana na kukosekana ndege ya kuuchukua msafara wote kwa pamoja.
Simba SC ambayo Agosti 8, itamenyana na mabingwa wa Rwanda, Rayon Sport Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika kilele cha tamasha la Simba Day
Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Sunday Manara amesema kwamba kikosi kinarejea kikiwa kimeiva na kipo tayari kabisa kwa msimu mpya wa ligi kuu na michuano mingine ya ndani na ya kimataifa.
“Wachezaji wetu wapo fiti na kwa mazoezi waliyoyafanya Afrika Kusini walipokwenda kuweka kambi na tumejiandaa vizuri kwenye kuelekea mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Rayon Agosti 8 ikiwa ni sherehe yetu ya kila mwaka ya siku ya Simba maarufu kwama Simba Day kwa kimombo na kimsingi nikwambie tu kwamba kikosi kinatarajiwa kutua kesho majira ya saa saba mchana na wengine watatua saa saba usiku,” amesema Manara
Pamoja na hayo, Manara ametaja pia viingilio katika mchezo wa Agosti 8 kuwa ni Sh.30,000 kwa VIP A, 20,000 kwa VIP B, 15,000 VIP C na 5,000 kwa viti vya mzunguko.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment