Pamoja na kufunga bao moja kwenye mechi ya kimataifa dhidi ya wa Comoro, lakini Yanga imeachana na ‘Mkata’ umeme na sasa inamsaka mbadala wake
Klabu ya Yanga imeamua kuachana na kiungo wake wa kimataifa wa Zambia Justine Zulu, baada ya kushindwa kuonyesha kiwango ambacho mabingwa hao wa ligi ya Vodacom walikitarajia kutoka kwake.
Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa amesema wameshazungumza na mchezaji huyo na wamekubaliana kuvunja mkataba huku wakimlipa fidia yake kwa awamu hadi kumaliza deni.
“Tumekaanaye chini na kukubaliana kwa pamoja na kuhusu malipo yake tutamlipa kwa awamu hadi ya kuyamaliza na kitu kizuri yeyemwenyewe amekubali kwahiyo mashabiki wa Yanga watambue kuwa msimu ujao hatutokuwa na Zulu tena,”amesema Mkwasa.
Kocha huyo amesema kuwa baada ya kuachana na Zulu, wanachokiangalia hivisasa ni kutafuta mchezaji mweingine ambaye ataziba nafasi hiyo ambayo kwasasa itakuwa wazi.
Amesema bado hawajaamua kuwa watamtafuta kutoka ndani au nje ya nchi lakini swala hilo analiacha kwa Kamati ya Usajili chini ya Mwenyekiti wake Hussein Nyika, ambaye ndiyo kujua ni wapi aelekee na anaweza kufanikiwa mapema kabla ya muda wa usajili haujamalizika.
Zulu alicheza mechi ya kwanza akiwa na jezi ya Yanga wakati walipokutana na JKU ya Zanzibar kwenye mchezo wa kirafiki, aliingia kipindi cha pili akitokea benchi na katika mechi tisa alizoichezea Yanga tangu aliposajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili kiungo huyo amefunga bao moja pekee.
0 comments :
Post a Comment