Mbunge Kubenea alia na rafu za serikali ya JPM


SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam, amesema Watanzania wanakuwa maskini kwa sababu ya ubaguzi unaofanywa na serikali, anaandika Hellen Sisya.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana jioni katika eneo la Kimara Kilungule,
Mbunge huyo alisema kuwa  serikali imekuwa ikibagua shughuli za maendeleo.
Amesema serikali imeshindwa kupeleka miradi mbalimbali ya maendeleo kwa maeneo ambayo yanaongozwa na wapinzani.
Ametoa mfano kuwa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita kwamba  mradi huo haukuwa na ulazima wowote kwani serikali ilikuwa na uwezo wa kuuboresha uwanja wa ndege uliopo jijini Mwanza badala ya kujenga mwingine.
“Ni lazima nchi hii iache upendeleo, iache ubaguzi, viongozi ni lazima wawe mfano kwa wananchi, ukianza kubagua hawa wapinzani, hawa ni CCM, ndani ya wapinzani wanaishi CCM, ndani ya CCM wanaishi upinzani.” amesema Kubenea.
Aidha, Mbunge huyo alisema ni lazima serikali iache kuwalinda baadhi ya watu ili kuleta usawa mbele ya sheria badala ya kuangalia sura wala cheo cha mtu.
“Mwalimu Nyerere alituacha tukiwa wamoja, taifa hili limeachwa likiwa moja, leo linakatwa vipande vipande kwa chuki na uhasama usio na msingi. Kuna ubaguzi kwenye nchi.!!Mtu mmoja,wamefanya makosa pamoja, mmoja anapelekwa mahakamani, mwingine ameachwa .” amesisitiza Mbunge huyo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment