Wabunge wa CUF kurudi tena mahakamani

Mashaka Ngole, Wakili upande wa CUF ya Prof. Ibrahim Lipumba


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya kupinga kuapishwa kwa wabunge wa viti maalumu ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) walioteuliwa na Prof. Ibrahim Lipumba Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini, anaandika Hamisi Mguta.
Waombaji katika kesi hiyo namba 143 ni wabunge wa chama hicho waliovuliwa uanachama wa chama hicho na mwenyekiti huyo na baadaye kutenguliwa ubunge wao.
Jaji wa Lugano Mwandambo alitoa uamuzi wa kutupilia mbali kesi hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili.
Jaji Mwandambo amesema kuwa hoja zilizowasilishwa na upande wa mashtaka hazina miguu kisheria.
Awali wakili wa upande wa Mashtaka Peter Kibata aliwasilisha hoja ya zuio la kuapishwa kwa wabunge wanane walioteuliwa na Prof. Lipumba.
Upande wa Jamhuri ambao uliwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata ulipinga hoja hizo kwa madai kwamba kifungu kilichotumika kufungulia shauri hicho cha sheria za Uingereza ambapo hakiwezi kusimama endapo sheria za ndani zinasema juu ya sheria hiyo.
Naye wakili wa upande wa wabunge wateule wa Prof. Lipumba Mashaka Ngole alipinga zuio hilo.
Hata hivyo, wakili kibatala anatarajia kufungua tena upya mashtaka hayo mchana  huu baada ya kufanya marekebisho katika baadhi ya vipengele vya kisheria.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment