Tanzania kupeperusha bendera mjini London kesho

Timu ya Taifa ya Riadha inayoshiriki mashindano ya Dunia ya riadha yanayoendelea jijini London inaanza kibarua cha kuipeperusha bendera ya Tanzania kesho, Jumamosi 05 ambapo mwanariadha Failuna Abdi Matanga anatarajiwa kukimbia mbio za mita 10,000.
Mashindano hay yanatarajiwa kuonyeshwa kwenye runinga mbalimbali duniani.
Mbali na Failuna anayekimbia mita 10,000, Watanzania pia watawashuhudia wanariadha wengine watatu siku ya Jumapili wakijaribu bahati yao kuanzia saa nne asubuhi ambao ni Alphonce Felix Simbu, Ezekiel Jafari Ng’imba na Stefano Huche Gwandu watakaoshiriki mashindano ya mbio ndefu za kilomita 42.
Katika mashindano hayo maarufu duniani, Tanzania pia imewakilishwa na wanariadha wa kike ambao ni Sara Ramadhani Makera na Magdalena Crispin Shauri ambao nao watakimbia mbio za kilomita 42 saa nane mchana.
Wanariadha wengine wa mbio fupi za mita 5,000 ambao ni Emmanuel Giniki Gisamoda na Gabriel Gerald Geay wataiwakilisha nchi siku ya Jumatano Agosti 9 saa mbili usiku ikiwa ni raundi ya mchujo na iwapo watafuzu watashiriki fainali ya mita 5,000 siku ya Jumamosi Agosti 12 saa mbili usiku.
Wanariadha wote wanaoshiriki mashindano hayo ni wale waliofikia viwango vya Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF).
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment