Mbunge wa Bunda Mjini Kupitia CHADEMA, Ester Amos Bulaya, amemtaka Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba, kuwataja watu wanaofanya uhalifu ikiwepo kuwatishia maisha baadhi ya viongozi hapa nchini ikiwepo Nape Nnauye kwani anawajua.
Bulaya ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, na kusema kwamba Waziri anawajua watu hao lakini anaogopa kuwataja kwa kulinda kitumbua chake kuingia mchanga.



0 comments :
Post a Comment