Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa uamuzi katika kesi ya uchochezi ya dikteta uchwara inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Mwendesha mashtaka wa serikali, Inspekta Said Hamis amemweleza hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Godfrey Mwambapa kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya uamuzi mdogo kama mtuhumiwa ana kesi ya kujibu au la, lakini imeshindikana kutokana na Lissu kuwa kwenye matibabu katika hospitali ya Nairobi.
Katika kesi hiyo Lissu anadaiwa Julai 28, mwaka jana katika viwanja vya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu alitoa kauli za uchochezi kuwa mamlaka ya serikali ni mbovu na ya kidikteta uchwara, akidai inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote.



0 comments :
Post a Comment