Chama cha Demakrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka serikali kuweka wazi utaratibu unaosemwa ulifuatwa na CCM kufanya mkutano wao wa chama Ikulu jijini Dar es salaam, ili kila mmoja ajue iwapo atahitaji kwenda kufanya mkutano hapo.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje- CHADEMA bwana John Mrema, amesema kama ukumbi wa Ikulu unaruhusiwa kufanyika mkutano na mtu yeyote, basi waweke wazi utaratibu na bei ili wengine nao wakiwa na vikao vyao wasisite kwenda ili kuongeza pato la taifa