
Wizara ya Nishati Tanzania imewaomba radhi wananchi kwa hitilafu ya umeme iliyojitokeza kuanzia Oktoba 25 – 26 kutokana na kukatika kwa waya katika bwawa la kufua umeme Kidatu.
Taarifa hiyo iliyotumwa kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa hitilafu hiyo imesababisha mikoa ambayo inapata umeme wa gridi ya taifa kuathirika kwa kukosa umeme, na unatarijiwa kutengemaa hapo kesho Oktoba 27 saa 5 asubuhi.
Taarifa hiyo imeendelea kwa kueleza kwamba hatua za dharula zinaendelea kuchukuliwa ili kumaliza tatizo hilo, huku ikiendelea kupambana kuhakikisha nchi inapata umeme wa uhakika
0 comments :
Post a Comment