Hali Ilivyo Baadhi Ya Maeneo Katika Upigaji Kura uchaguzi Wa Madiwani Leo

Rungwe. Ulinzi umeimarishwa kila kona katika Kata ya Ibighi Wilaya ya Rungwe wakati wananchi wakiendelea kupiga kura za udiwani wa kata hiyo.
Katika kata hiyo CCM na Chadema wameweka walinzi wao kwenye maeneo jirani ya vituo vya kupigia kura.

Msimamizi wa Uchaguzi Mbeya, Stevin Mwakingwe amesema hadi sasa upigaji kura unaendelea vizuri huku utulivu ukitawala katika kituo vyote vya kupigia kura.

Mwakingwe amesema vituo vyote 13 vya kupigia kura vimefunguliwa na kuanza kazi saa1:00 asubuhi na watu wanazidi kujitokeza kwa wingi.

“Nashukuru hadi muda huu watu wanaendelea kupiga kura kwa utulivu kabisa kama unavyoona mwenyewe (mwandishi). Sijapokea malalamiko yoyote kutoka kwa wapiga kura, wasimamizi au mawakala," amesema Mwakingwe.

Amesema kata hiyo ina wapiga kura 4,591 ambao wanatarajia kupiga kura leo Jumapili.

Wagombea udiwani Kata ya Ibighi wapo watano ambao ni Suma Fyandomo (CCM),  Lusubilo Simba (Chadema), Geoffrey Mwakajinga (UDP), Emmanuel Mwasilembo (DP) na Grace Ngalaba (CUF).
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment