Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan, amekwenda hospitali kumuona mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu, ambaye amelazwa kutokana na kupigwa risasi.
Mama Samia ambaye alikuwa jijini Nairobi kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, aliwasili hospitalini hapo jioni hii akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chana.
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu anakuwa kiongozi wa kwanza mkubwa kitaifa kwenda kumuona mbunge huyo ambaye yupo hospitalini hapo tangu Septemba 7 alipopigwa risasi na watu ambao hawajajulikana mpaka sasa.
Mama Samia ambaye alikuwa jijini Nairobi kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, aliwasili hospitalini hapo jioni hii akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chana.
0 comments :
Post a Comment