Abiria Waonywa Kukata Tiketi Kwa Wapiga Debe

 

BARAZA la Ushauri na Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, limewataka wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika ikiwamo Polisi endapo watatozwa nauli tofauti na zilizopangwa.

Hatua hiyo inafuatia katika kipindi hiki cha mwezi Desemba nauli hasa kwa wasafiri waendao mikoani wanaotumia usafiri wa mabasi hupanda maradufu.

Wito huo umetolewa  leo jijini Dar es Salaam  na katibu mtendaji wa baraza hilo, Dk Oscar Kikoyo wakati akizungumzia hali ya usafiri katika kipindi cha sikukuu za krismas na mwaka mpya (2018).

“Baadhi ya watoa huduma ambao si waaminifu katika kipindi hiki kama  ni njia ya kuvuna zaidi kutoka kwa watumiaji kinyume na masharti ya leseni zao. Hivyo wasafiri wachukue hatua ya kuwapeleka polisi au katika mamlaka husika za usafirishaji, “amesema.

Amesema kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri, baadhi ya abiria hukubali kulipa zaidi ili wapate kusafiri.

Dk. Kikoyo ameukumbusha Umoja wa  wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani(Taboa),kufuata masharti ya leseni zao na kutoza nauli zilizoidhinishwa na  Sumatra.

“Baraza linawahimiza wamiliki, kuwahimiza wafanyakazi wao wanaokata tiketi katika vituo mbalimbali kuwa waaminifu kwa waajiri  na wateja wao,”amesema.

Amesema wananchi wasinunue tiketi kwa wapiga debe au vishoka katika kituo cha mabasi Ubungo au vituo vingine pamoja na kuhakikisha jina na kiwango sahihi alichotoa na kilichoandikwa.

Ameongeza magari yaliyopewa vibali vya muda kusafirisha abiria mikoani yakaguliwe kwa kina kabla ya kukata tiketi.

Kuhusu wanaobeba mizigo katika vitua vya mabasi amesema ‘’ Kwanza mkubaliane bei kabla hajabeba mizigo  pia akupe au akuonyesha kadi yake yenye namba iliyoandikwa kwenye koti lake nyuma, mbele na kwenye toroli lake.’’
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment