Simba Na Lipuli Mgogoro Wa Usajili Bado Unafukuta Kuhusu Asante Kwasi

 
KLABU ya Soka ya Lipuli inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) imesema mlinzi Asante Kwasi bado ni mchezaji halali wa kikosi hicho na alitakiwa kuripoti kambini tangu Desemba 16 mwaka huu lakini hajafanya hivyo hadi sasa. 
Lipuli kupitia kwa msemaji wake Clement Sanga imeeleza kusikitishwa kwake na taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa mchezaji huyo raia wa Ghana amejiunga na Klabu ya Simba, Sanga amesema taarifa hizo sio za kweli kwani bado anamkataba na timu hiyo licha ya kutoonekana klabuni hapo (kuingia mitini).
 

“Asante Kwasi tulimpa ruhusa ya kuhudhuria msiba wa baba yake nyumbani kwao Ghana, alitakiwa kurudi Desemba 16 mwaka huu na tulifuata taratibu zote ikiwemo kumtumia pesa ya tiketi ya ndege pamoja na mshahara wa mwezi uliopita, lakini hadi sasa hajafika hivyo tunashindwa kuelewa”, amesema Sanga.
 

Siku za hivi karibuni kumekuwepo na taarifa mbalimbali kuwa mlinzi huyo ambaye amefunga mabao matano hadi sasa kwenye Ligi Kuu, amesajiliwa na Simba japo vinara wa ligi hiyo hawajatoa taarifa juu ya usajili huo.
 

Tayari Lipuli imeshaweka hadharani majina ya wachezaji walioachwa na waliosajiliwa kwenye dirisha dogo ambapo walioachwa ni Waziri Ramadhani, Mussa Ngunda, Machaku Salum, Melvin Alistoto, Dotto Kayombo  na Ahmeid Manzi.
 
Waliosajiliwa ni Jamal Mnyate kwa mkopo kutoka Simba, Adam Salamba kutoka Stand United, Alex Ntiri kutoka Mbao FC ambaye ni raia wa Ghana, Miraji Mwilenga na Awadi Mauya kutoka Mufindi United pamoja na  Steven Mganga kutoka Pamba FC.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment