Kenya Mbunge Atishia Kujiuzulu

Mbunge wa Nyando nchini Kenya Jared Okello ametishia kujiuzulu ikiwa kiongozi wa upinzani ( NASA) Raila Odinga hataapishwa kuwa Rais wa wananchi.

Mbunge huyo ambaye anatokea chama cha ODM amesema atachukua hatua hiyo kwa sababu anaamini kuwa mwanasiasa huyo mkongwe ndiye alishinda katika uchaguzi mkuu wa Agosti 8 mwaka huu, lakini akapokonywa ushindi.

“Nilienda bungeni si kuwa upande wa upinzani ila kuunga mkono sera za Rais Raila Odinga huku akiendesha majukumu yake kutoka Ikulu. Nimechunguza kwa makini jinsi kura zilivyopigwa mnamo Agosti 8 na kung’amua kuwa Raila alishinda kwa kura nyingi mno, kwa hivyo ikiwa hataapishwa baada ya majuma mawili yajayo, nitajiondoa kuwa mbunge wa Nyando. Siwezi kuketi bungeni na watu waliopanga njama ya kumpokonya Bw Odinga ushindi ili aendelea kukaa kwenye baridi,” amesema mbunge huyo.

Hivi karibuni kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amesema kwamba lengo lake la kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo liko pale pale, na ataapishwa ili kuwahudumia wananchi waliomchagua, kitendo ambacho kimeanza kupingwa na serikali kwani tayari yupo Rais aliyeapishwa kwa mujibu wa katiba ya nchi ya Kenya.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment