Marufuku Kufanya Mahubiri ,Biashara Ndani Ya Mabasi Ya Abiria

 
Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri wa nchi kavu na majini limepiga  marufuku wafanyabiasha na wahubiri kuendesha shughuli zao kwenye mabasi ya abiria.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Oscar Kikoyo amesema kwamba ndani ya basi si sehemu ya kufanyia biashara wala mahubiri, yeyote atakaekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua,pia amewaonya madereva na makondakta.

Mbali ya suala hilo, Katibu Mtendaji huyo  
amepiga marufuku kuonyesha video na kupiga miziki isiyozingatia maadili kwenye mabasi ya abiria. 

Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya watendaji kwenye mabasi ya abiria kuweka burudani mbalimbali zikiwemo filamu na maigizo wakati safari ikiendelea, lakini nyingine kati ya burudani hizo zinadaiwa kukiuka maadili ya mtanzania.

Dkt. Oscar Kikoyo amewataka abiria katika mabasi kutoa taarifa kwa vyombo husika endapo agizo hilo litakiukwa.

Katika hatua nyingine Dkt. Kikoyo amewataka wamiliki wa magari kuzingatia bei elekezi ya nauli inayotolewa na SUMATRA kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment