Wenger Azidi Kuponda Waamuzi Wa EPL


Kocha wa Arsenal Arsene Wenger kwa mara nyingine amejikuta akipishana na waamuzi EPL baada ya kumponda muamuzi wa mchezo wao wa jana kwamba haelewi ni kwanini muamuzi Anthony Taylor aliwapa tuta Chelsea.
Chelsea walipata penati hiyo baada ya Hector Bellerin kuinekana kama amemchezea vibaya Eden Hazard na Hazard akamfunga mkwaju huo wa penati na kumfanya kuhusika katika mabao 100 ya Chelsea (amefunga 63 na assist 37).
Thiery Henry kwa upande wake ameungana na muamuzi Anthiny Taylor na kusema kwamba Bellerin alionekana wazi kuukosa mpira na kumbughudhi Hazard, kosa ambalo Henry amesema ni penati ya wazi.
Kabla ya bao la Hazard tayari Arsenal walikuwa wakiongoza baada ya Jack Wilshaire kufunga bao lake la kwanza tangu mwaka 2015 huku hili likiwa bao lake la 8 katika jumla ya michezo 157 ya EPL aliyocheza.
Marcos Alonso aliwapatia Chelsea bao la pili ambalo linamfanya kuwa mlinzi mwenye mabao mengi EPL (6) kabla ya Hector Bellerin naye kuisawazishia Arsenal huku ikiwa ni bao lake la kwanza EPL na mchezo kuisha kwa sare ya mbili mbili
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment