Mgombea Udiwani Wa Chadema Aliyejeruhiwa Vibaya Apelekwa Dar Kwa Matibabu Zaidi

Katibu mwenezi wa Chadema Muleba Kusini, Hamisi Yusufu amesema hawezi kutaja alikolazwa mgombea huyo kwa sababu za kiusalamaMuleba. Viongozi wa Chadema wilayani hapa Mkoa wa Kagera, wamesitisha shughuli za kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa Buhangaza Mchungaji Nelson Athanasio Makoti  ili kupata nafasi ya kushughulikia matibabu yake baada ya kuhamishwa Hospitali ya Kagondo hadi Dar es Salaam kwa matibabu.
Katibu mwenezi wa Chadema Muleba Kusini, Hamisi Yusufu amesema hawezi kutaja alikolazwa mgombea huyo kwa sababu za kiusalama kutokana na hali ya upepo ulivyo kisiasa hapa nchini.
Amesema kampeni za uchaguzi wa udiwani Kata ya Buhangaza, zitaendelea kesho.
"Suala la wapi mgombea  amelazwa  msemaji wake anaweza kuulizwa Tumaini  Makene  lakini kwa taarifa nilizopokea asubuhi ya leo ameonyesha mabadiliko tofauti na ilivyokuwa Kagondo," amesema Yusufu.
Hata hivyo, amesema wananchi wanatakiwa kuwa wavumilivu na kwa sasa Chadema hawaelekezi tuhuma zozote kwa kundi lolote la kisiasa.
Amesema  jukumu kubwa ni vyombo vya dola kufanya kazi ya kuchunguza na kubaini waliohusika kwa kusababisha mgombea kuathirika kiafya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Isack Msangi amesema katika mahojiano na Makoti na ndugu zake na wananchi hakuna mtuhumiwa anayeshikiliwa japo upelelezi unaendelea.
Msangi amesema saa tisa alasiri ya leo jeshi hilo litatoa ufafanuzi kuhusu mwenendo wa kufuatilia tukio la mgombea huyo na mahali alipo ili kuwaweka sawa wananchi wanaofuatilia kinachofanyika dhidi ya mpendwa wao.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment