Video:Jaji Anaesikiliza Kesi Ya Lipumba ,Bodi Ya Wadhamini CUF Yataka Ajitoe





Kesi iliyofunguliwa  na Bodi ya wadhamini CUF dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, Profesa Ibrahimu Lipumba na wanachama 11 wa chama hicho imesikilizwa leo December 6 2016 mahakama kuu kanda ya Dar es salaam.
Wakili wa bodi ya wadhamini CUF, Juma Nassoro amesema Jaji anayesimamia kesi, Jaji Kihiyo ajiondoe kwenye kesi hiyo huku akitaja hoja kuu mbili, ya kwanza amesema inajengwa na kesi hiyo wakati ilipotajwa Novemba 11, mwaka huu ambapo Jaji Kihiyo aliibua hoja iliyohusu uhalali wa wadhamini ambayo ilikuwa na muelekeo wa kuwaonyesha wadaiwa nini wafanye.
Aidha hoja nyingine ni kauli iliyotolewa na Jaji huyo kwamba shauri hilo limefunguliwa kwa haraka haraka. Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Sakieti Kihiyo anatarajia kutoa uamuzi wa kujitoa ama kutojitoa kuendelea kuisikiliza kesi iliyofunguliwa na Bodi ya Baraza la Wadhamini la Chama cha Wananchi ‘CUF’, Desember 14, mwaka huu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment