Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, Bw.Mussa Juma Assad akizungumza
wakati wa hitimisho la mkutano wa siku mbili wa Bodi hiyo uliofanyika
hapa Umoja wa Mataifa kuanzia Julai 22-23. Kushoto kwake ni Bw. Fransis
Kitauli, Mkurugenzi wa Ukauzi wa Nje na Mwenyekiti wa Kamati ya
Operesheni za Ukaguzi ( AOC) Akiwa Mwenyekiti wa AOC Bw. Kitauli
ambaye alishika nafasi hiyo tangu mwaka 2012 amefanikisha utoaji wa
ripoti za ukaguzi za Umoja wa Mataifa kwa miaka mitatu mfululizo.
Wajumbe
wa Bodi ya Ukaguzi kutoka kushoto, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali
ya India, Bw. Shashi Kant Sharma, Sir Amyas Morse, Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu kutoka Serikali ya India na Bw. Mussa Juma Assad, Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya Tanzania wakitia saini zao katika ripoti
28 za ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa zilizorejewa na
kupitishwa na Bodi hiyo wakati wa mkutano wake wa siku mbili. ripoti
hizo ni matokeo ya kazi kubwa ya Bodi hiyo.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Bodi wakiwa pamoja na wataalamu wao na wajumbe kutoka Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.
Ujumbe wa Bodi ya Uingereza ukiongozwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Sir Amyas Morse.
Ujumbe wa Bodi ya India ukiongozwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Bw. Shadhi Sharma.
Ujumbe
wa Bodi ya Tanzania ambao ni kutoka kushoto Jerome Francis, Naibu
Mkurugenzi ukaguzi wa Nje, Bw. Salhina Mkumba, Naibu Mkurugenzi,
Ukaguzi wa Nje na ambaye amefanya kazi kwa karibu sana na Bw. Fransis
Kitauli tangu Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
ilipoteuliwa kuingia kwenye Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa wa
mwisho ni Bw. Athuman S. Mbuttuka, Naibu Mkaguzi Mkuu.
Na Mwandishi Maalum, New York
Bodi
ya Ukaguzi wa Hesabu za Mashirika ya Umoja wa Mataifa , imemaliza
mkutano wake wa siku mbili kwa kurejea na kupitisha taarifa 28 za
ukaguzi.
Taarifa
22 kati ya hizo zitawasilishwa mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa na sita zitawasilishwa kwa Mamlaka na vyombo vingine.
Mkutano
huo umefanyika hapa Umoja wa Mataifa chini ya Uenyekiti wa
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Bw. Mussa Juma Assad.
Wajumbe
wengine wa Bodi ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya
Uingereza Sir Amyas Morse na Bw. Shashi Kant Sharma, Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya India.
Akizungumza
mara baada ya kutia saini taarifa hizo, jukumu lililofanywa kwa
pamoja na wadhibiti na Wakaguzi hao watatu, Bw. Mussa Juma Assad
amewashukuru wajumbe wenzie kwa kazi kubwa na nzuri ambayo
wameifanya katika siku hizo mbili pamoja na ushirikiano mzuri
waliompatia.
“
Nichukue fursa hii kuwashukuru sana kwa kazi hii nzuri na ushirikiano
mkubwa mlionipatia, ushirikiano ambao umetuwezesha kukamilisha kazi hii
kwa wakati na muda muafaka”, akasema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za serikali Bw. Assad.
Wakijibu
shukrani hizo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya
Uingereza, Sir Amyas Morse alimshukuru Mwenyekiti kwa uongozi wake na
upeo mkubwa ikiwa ni pamoja na ushirikiano wake kwa wajumbe wenzie.
Akatumia
pia fursa hiyo kumpongeza na kumshukuru kwa moyo wa dhati, Bw.
Fransis Kitauli ambaye kwa miaka mitatu akiwa Mwenyekiti wa Kamati
ya Operesheni amefanikiwa kutolewa kwa ripoti za ukaguzi bila kukosa.
Sir
Morse amemuelezea Bw. Kitauli kama Mkurungezi na Mwenyekiti ambaye
ameonyesha weledi mkubwa na kujituma kwa hali ya juu katika
utekelezaji wa majukumu yake amekuwa Mkurugenzi anayemwakilisha
Mkaguzi Mkuu hapa Umoja wa Mataifa kwa uadilifu wake, na weledi
mkubwa katika utekelezaji na usimamizi wa majukumu yake na akamtakia
kila la kheri arejeapo Tanzania.
Kwa
upande wake Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali ya India, Bw.
Shashi Sharma, pamoja na kumshukuru Mwenyekiti kwa uongozi wake mahili
naye alimpongeza na kumshukuru Bw. Fransis Kitauli kwa uhodari wake,
kujituma na kazi kubwa aliyoifanyia katika utekelezaji na
usimamizi wa majukumu ya Bodi hiyo.


0 comments :
Post a Comment