Wednesday, July 8, 2015
Nkupamah blog
WANACHAMA watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wametangaza kuingia katika kinyang’anyiro cha kuomba kuteuliwa katika Ukawa kuwania ubunge jimbo la Tabora Mjini.
Walitambulishwa jana katika mwendelezo wa mikutano ya hadhara
iliyoandaliwa na uongozi wa chama hicho mkoa ambao jana ulifanyika
katika kata ya Mpera katika Manispaa ya Tabora.
Wanachama wanaowania kuteuliwa na chama hicho ni Profesa Hamba
Makambi, Raymond Maganga, Said Mwakasekela, Furaha Kisanji na Peter
Mkufya.
Mwanachama mwingine, Rehema Raphael anawania viti maalumu wanawake.
Wagombea hao wa chama hicho watachujwa Julai 25 na kubaki mmoja
atakayepambanishwa na mwingine kutoka kila chama kinachounda ukawa kabla
ya kupatikana mgombea atakayepeperusha bendera ya ukawa kwenye jimbo la
Tabora Mjini linaloongozwa na Ismail Rage wa CCM.
Mratibu wa Kanda wa Chadema, Christopher Nyamwanji alisema viongozi
wasiokuwa na dhamira ya kuwakomboa watanzania ndio wameifikisha nchi
pabaya.
Alieleza kuwa pamoja na mkoa kuwa na misitu katika maeneo mengi, inashangaza kuona wanafunzi wakikaa chini madarasani.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment