Bendera ya Burundi
Muungano
wa Ulaya EU umeanza kikao maalum kujadili uwezekano wa kukata msaada
wake nchini Burundi. Inakisiwa kuwa fedha kutoka muungano huo unafikia
zaidi ya nusu ya bajeti nzima ya Burundi ya kila mwaka.
Federica Mogherini wa EU
Mkuu wa
masuala ya kigeni wa Muungano wa EU Federica Mogherini, ameelezea
wasiwasi wake juu ya ghasia zilizototokea nchini humo kabla ya kufanyika
uchaguzi wa rais, na ametilia shaka iwapo serikali itakayoundwa baada
ya uchagzui huo itakuwa wakilishi ya taifa nzima.
Upande wa uchaguzi ulisusia kura hiyo iliyofanywa siku ya Jumanne. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Ijumaa hii.
Uamuzi wa
Rais Pierre Nkurunzinza kuwania urais kwa muhula wa tatu umetajwa
kwenda kinyume na mkataba waliosaini mjini Arusha miaka kumi na tano
iliyopita, ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mingi.
ghasia katika barabara za Burundi
Ghasia
zimezuka nchini humo tangu rais Pierre Nkurunzinza kutangaza kuwania
kiti hicho ambapo zaidi ya watu laki moja wamikimbia nchi hiyo huku
makumi ya maelfu wengine wakiuawa katika maandamano.
Juhudi kadhaa za kuleta upatanishi kati ya makundi hasimu zimeambulia patupu.


0 comments :
Post a Comment