Bendera ya Marekani
Polisi
katika jimbo la Louisiana nchini Marekani wamesema kuwa mtu mmoja
aliyejihami kwa bunduki amewafyatulia risasi raia katika ukumbi wa
sinema na kumuua mtui mmoja. Watu wengine ssita wamejeruhiwa , na
mshambuliaji mwenyewe pia amejiua.
Walioshuhudia
wanasema kuwa walimuona mtu mmoja, mzungu wa umri wa miaka 50 au zaidi,
amejitokeza kunako dakika ishirini baada ya filamu kuanza , filamu ya
Train wrek, na kisha kuanza kufyatua risasi kiholela. Mmoja anasema kuwa
alisikia mlipuko kama vile baruti.
Polisi wazingira eneo la ufyatiliaji wa risasi Marekani
Polisi wamezingira eneo la tukio huku Gavana wa jimbo hilo akisema kuwa anaelekea huko kujikagulia mwenyewe hali iko vipi.
Hili
imetokea saa chache tu baada ya Rais Barack Obama kuzungumzia tatizo la
udhibiti wa silaha nchini Marekani. Katika mahojiano maaluma na BBC ,
Rais Obama amesema kushindwa kudhibiti silaha nchini mwake ni jambo
lililomsononesha katika utawala wake.
Bunduki za Marekani zinahitaji udhibiti
Amesema
Marekani ni nchi pekee iliyoendelea ambayo haina sheria ya kutosha
kuhusu usalama wa silaha, hata wakati huu ambapo kumekuwa na marudio ya
matukio ya mauaji.
Obama
amesema magaidi wamewaua chini ya wamarekani 100 tangu shambulio la
kigaidi la Septemba 11, lakini waliouawa kwa matukio ya kutumia silaha
ni makumi kwa maelfu katika kipindi hicho.
Rais Obama akihutubia bunge la Congress juu ya silaha
Rais
Obama alijaribu kusukuma mbele sheria ya udhibiti wa silaha baada ya
tukio la mauaji kwenye shule moja inayojulikana kwa jina la Sandy Hook
School mwaka 2012, lakini sheria hiyo ya kubana matumizi ya silaha
ilikataliwa na bunge la Congress.


0 comments :
Post a Comment