Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa mjini Iringa, Nuru Hepautwa akizungumza jambo kwenye moja ya mkutano wa chama
Na Friday Simbaya, Iringa
KADA
maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa mjini Iringa, Nuru Hepautwa
amesema anafahamu maumivu yaliyotokea kwa wana CCM baada ya kuachia
jimbo hilo mikononi mwa Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2010 lakini
akaahidi kuyamaliza endapo atapewa ridhaa hiyo.
Hepautwa
ambaye pia ni mfadhili wa mashindano ya soka yaliyojizolea umaarufu
mjini Iringa ya Hepautwa Cup alitoa mchango huo jana wakati akijinadi
kwa wanachama katika Kata ya Kitwiru Jimbo la Iringa mjini.
MFANYABIASHARA
huyo alitangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Iringa Mjini hivi
karibuni katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu
kwa kupitia tiketi ya chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM).
Hepautwa
ambaye pia ni Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi
(UVCCM) Iringa Mjini alisema anafahamu maumivu yaliyotokea kwa wana CCM
baada ya kuachia jimbo hilo mikononi mwa Chadema katika uchaguzi lakini
akaahidi kuyamaliza endapo atapewa ridhaa hiyo.
Kwa
mwaka wa tano sasa, jimbo la Iringa Mjini limeendelea kuongozwa na
Mchungaji Peter Msigwa aliyechaguliwa kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Akizungumzia
vipaumbele vyake endapo atapewa ridhaa hiyo, Hepautwa alivitaja kuwa ni
pamoja na kubuni vyanzo vipya vya ajira kwa vijana na kuboresha huduma
katika sekta mbalimbali zikiwemo za afya, maji, elimu, miundombinu ya
barabara na biashara.
Kwa
upande wa sekta ya biashara alisema mpango wake ni kuwashawishi
wafanyabiashara wenye uwezo mkubwa kujenga viwanda vya mazao ya kilimo,
kutenga maeneo ya wafanyabiashara wadogo na kuufanya mji wa Iringa kuwa
mji wa kibiashara.
“Nataka
kuona Iringa unakuwa mji wa biashara za aina zote, magari, vipuri,
mitambo, nguo, vyakula na nyinginezo ili waliojirani na CCM wasiende
tena Dar es Salaam ili sehemu ya kununua mali wanazohitaji kwa jumla iwe
Iringa,” alisema.
Alitaja
biashara nyingine zinazoweza kufanywa na wakazi wa Iringa Mjini kuwa ni
pamoja na ya kuongoza na kusafirisha watalii ili kuiongezea msukumo wa
kutosha.
“Kule
kaskazini, vijana wengi kama sisi wamenufaika na mapato yatokanayo na
utalii kwasababu wamethubutu kuwekeza katika sekta hiyo. Nataka kuona na
sisi wa Iringa tunatumia ujirani wetu na hifadhi ya Taifa ya Ruaha
kuchangamkia fursa hiyo,” alisema.
Katika
afya alizungumzia namna atakavyosaidia kuboresha huduma hasa za mama na
mtoto, mapambano ya virusi vya Ukimwi na upatikanaji wa vifaa tiba na
dawa katika vituo vyote vya kutolea huduma.
Katika
Jimbo la Iringa mjini, mkoani Iringa chama hicho kimeandaa mikutano kwa
wagombea ubunge wote ya kuwatambulisha kwa wanachama ikiwa sehemu ya
pili ya mchakato ya kumpata mgombea pekee atakaye peperusha bendera ya
chama hicho kwa kushindana na vyama vya upinzani katika Uchaguzi Mkuu
Oktoba mwaka huu.
Jumla
ya wagombea ubunge 13 Iringa mjini waliochua na kurudisha fomu na
wameanza safari ya kuwatambulisha kwa wanachama katika matawi 81 ya CCM
Jimbo la Iringa Mjini.
Wana
CCM hao wanaoomba nafasi ya ubunge ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Iringa Jesca Msambatavangu, Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Frederick
Mwakalebala na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mahamudu Madenge.
Katika
orodha hiyo yupo pia Dk Yahaya Msigwa, Nuru Hepautwa, Addo November
Mwasongwe, Adestino Mwilinge, Frank Kibiki, Aidani Kiponda, Peter
Mwanilwa, Fales Kibasa, Michael Mlowe na Balozi mstaafu Dk. Augustine
Mahiga.
Addo November Mwasongwe,
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu
Fales Kibasa
Frank Kibiki
Balozi mstaafu Dk. Augustine Mahiga
Michael Mlowe
Dk Yahaya Msigwa
Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Frederick Mwakalebala
Peter Mwanilwa
Aidani Kiponda (Weekend)
0 comments :
Post a Comment