Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika DRC Bw.
Martin Kobler akiwasilisha taarifa mbele ya Baraza Kuu la Usalama la
Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu,
hali ya usalama na mkakati wa kupunguza walinzi wa amani. na
Kueleza kwamba utekelezaji wa mamlaka ya MONUSCO unahitaji ushirikiano
endelevu kati yake na mamlaka za DRC
Mwenyekiti wa Kamati ya Vikwanzo dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, Dina Kawar akiwasilisha taarifa ya Kamati yake mbele ya Baraza
Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambapo pamoja mambo mengine
ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumkamata
na kisha kumpeleka nchi Uganda kiongozi la kundi la wanamgambo la
Allied Democratic Forces ( ADF) Bw. Jamil Mukulu ambaye alikuwa katika
orodha ya watu waliowekewa vikwazo na Kamati hiyo.
Na Mwandishi Maalum , New York
Uwezo wa Misheni ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo ( MONUSCO) wa kutekeleza mamlaka yake kikamilifu utategemea
zaidi ushirikiano na uhusiwano wake na mamlaka za nchi hiyo.
Hayo yameelezwa na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
katika DRC, Bw. Martin Kobler wakati alipowasilisha taarifa yake
mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa siku
ya jumaane.
Taarifa Bw. Kobler kwa Baraza hilo ilihusu maeneo matatu ambayo ni
uchaguzi mkuu utaotarajiwa kufanyika mwakani, hali ya usalama na
mkakati wa upunguzaji wa idadi ya walinzi wa Amani.
“ Mafanikio ya utekelezaji wa mamlaka yetu unategemea na kuendelea kwa
majadiliano na ushirikiano na serikali na hususanu kuhusu hali ya
usalama katika eneo la Mashariki na Mchakato wa Uchaguzi.
Akielezea zaidi kuhusu hali ya usalama, Mwakilishi wa Katibu Mkuu,
ameliambia Baraza kwamba, kuna matumaini katika baadhi ya maeneo.
Akibainisha juu ya operesheni zinazoendelea dhidi ya kundi la
wanamgambo la Force de Resistance Patriotique en Ituri ( FPRI) na
zinazofanywa na Jeshi la DRC ( FARDC) kwa kusaidiwa na MONUSCO.
“ Wakati kipaumbele ni kuhakikisha kuwa kundi hili linasalimisha
silaha kwa hiari, matumizi ya nguvu ilibidi yafanyike baada ya kunvujwa
mara tatu muda wa mwisho ambao kundi hilo lilipashwa kusalimisha
silaha zake kwa hiari” amesema Bw. Kobler
Kuhusu operesheni ya pamoja dhidi ya kundi la Force Democratique de
Liberation du Rwanda ( FDLR) katika maeneo ya Kivu Magharibu, Kivu ya
Kusini na Katanda amsema operesheni hiyo imesimama kwa zaidi ya
miezi mitano.
Amefafanua kuwa kusimama kwa operesheni hiyo ambayo ilitakiwa ifanywe
na FARDC kwa kusaidiwa na MONUSCO licha ya kwamba pamoja na mambo
mengine kulitoka na hoja ya awali kuhusu haki za binadamu bali sasa
limekwenda mbali zaidi ya hapo.
Akaongeza kwamba wakati MONUSCO ikirejea na kufanya tathmini kuhusu
haki za binadamu ilikuwa inatafuta njia ya namna ya kuendeleza
ushirikiano kupitia mpango uliopo sasa.
Akielezea zaidi kuhusu hali ya usalama, Bw. Martin Kobler amesisitiza
kuwa wakati serikali ya DRC imepiga hatua kubwa katika kurejesha hali
ya Amani katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Bado wananchi wa eneo
la Mashariki ya nchi hiyo maisha yao yanategemea sana huruma ya
makundi ya wanamgambo wenye silaha.
Pamoja na mafanikio ya kupunguza nguvu ya FDLR katika baadhi ya
maeneo waliyokuwa wakiyakalia, jeshi la DRC limejikuta katika mazingira
magumu ya kuyadhibiti na kuyashikilia maeneo yaliyokombolewa na
kwamba hakuna muda wa kusubiri.
Kuhusu uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka
2016, Bw. Kobler amesema wajibu wa kuhakikisha kwamba uchaguzi huo
unakuwa wa huru, haki na wazi ni wa serikali yenyewe ya DRC
Akaongeza kwamba tajio la haraka katika kuhakikisha kwamba uchaguzi
utafanyika kwa wakati ni fedha , kalenda sahihi ya uchaguzi,
uboreshaji wa daftari la wapiga kura na utoaji wa fursa kwa vyama vya
upinzani. Akamsifu Rais Kabila kwa kupanua wigo wa majadiliano na
wadau mbalimbali katika kipindi cha kuelekea uchaguzi.
Katika hatua nyingine. Mwakilishi wa Jordan na ambaye ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Vikwanzo dhidi ya DRC, Dina Kawar , ameishukuru Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumkamata na kisha kukubali
kumpeleka nchini Uganda kiongozi wa Kundi la Allied Democratic
Force ( ADF) Bw. Jamil Mukulu
Ametoa shukrani hizo wakati naye alipokuwa akiwasilisha taarifa ya
Kamati yake mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa




0 comments :
Post a Comment