Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Seif Suleman akiwa
katika bandari ya Zanzibar kuupokea Ujumbe wa Madaktari kutoka Jumuiya
ya Watanzania Washington ukiwa wenyeji wa PBZ na Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa na Diaspora Zanzibar wakiwa katika bandari hiyo kuupokea kwa
ajili ya kutoa huduma ya Afya kwa Wananchi wa Zanzibar katika hospitali
ya Mnazi mmoja kesho, Kwa muji wa Mkurugenzi wa Idara hiyo Ndg Adila
Hilal Vuai amesema utatoa huduma ya Uchunguzi wa Satatani ya Maziwa kwa
Kinamama, Kisukari, Presha Meno na tiba nyengine kwa wananchi wa
Zanzibar watakaofika katika hospitali hiyo kupata huduma hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa PBZ Ndg Seif Suleiman akisalimiana na mmoja wa
madaktari hao Bingwa walipowasili katika bandari ya forodhani wakitokea
Dar -es- Salaam walikuwa wakitowa huduma hizo kwa Wananchi.katikati
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Ndg Adila Hilal
Vuai. wakiwapokea wageni wao.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washington Ndg Iddi Sandaly akizungumza
na Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBA) Ndg Seif
Suleiman alipowasili katika bandari ya Zanzibar wakitikea Dar na Ujumbe
wa Madaktari 17 watakuwa Zanzibar kwa kutoa huduma ya Tiba kwa Wananchi
wa Zanzibar katika hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kesho asubuhi.
Madktari kutowa Washington DC,MD,VA wakiwasili katika bandari ya
Zanzibar wakitokea Dar-es-Salaam baada ya kutoa huduma ya Tiba.kwa
Wananchi wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Diaspora Zanzibar
Ndg Adila Hilal Vuai akiwa na mmoja wa Madaktari hao Dr. Hailu
wakizungumza wakati alipowasili katika bandari ya Zanzibar jioni hii
tayari kwa kutowa huduma ya matibabu kwa Wananchi wa Zanzibar katika
hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kesho. wakitoka katika bandari ya
Zanzibar.
Madaktabi Bingwa wakifurahia mandhari ya Zanzibar wakiwa katika
bandari ya Malindi Zanzibar baada ya kuwasili katika Visiwa vya Marashi
ya Karafuu.
Watanzania wanaoishi Washinton Bi Asha Nyanganyi akiwa na Rais wa
Jumuiya ya Watanzania Washinton Ndg Iddi Sandaly.wakiwa katika bandari
ya Zanzibar walipowasili leo jioni wakitokea Dar,


0 comments :
Post a Comment