Itakumbukwa Mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu katik
a
hotuba yangu niliyo iwasilisha kwa wanausalama mitandao tulipo kutana
jijini Johannesburg mbali na mambo mengine nilihimiza sana ushirikiano
baina yetu kwani wahalifu mtandao wamee
ndelea kua mbele yetu kutokana na
ushirikiano mkubwa waliokua nao. Ushirikiano unao mabatana na kusambaza
vitendea uhalifu mtandao bure auu kwa gharama nafuu mitandaoni.
Baada ya kulizungumza hili
laushirikiano wazungumzaji wengine wote walionekana kuniunga mkono na
hatimae kuonekana ni swala muhimu lakufanyiwa kazi mapema. Nafarijika
kuona Uingereza tayari mukuu wake wa CERT ametilia mkazo kauli hii (Ya
ushirikiano) kupitia kikao kilicho malizika London ambapo taarifa kamili
kuhusiana na hili inaweza kusomeka kwa “KUBOFYA HAPA”
Aidha, Marekani na Israel baada ya
kutia saini makubaliano ya kuboresha ushirikiano katika maswala ya
usalama mitandao paliambatana na kuhimiza mataifa mengine kuona umuhimu
wa kushirikiana katika vita hii ya uhalifu mtandao.
Nilipata kuzungumza tena katika
mkutano wa wanausalama Nchini Cyprus ambapo pia nilizungumza kwa mara ya
kwanza kuhusiana na ushirikiano huku nikipongeza umoja wa ulaya kwa
kuungana kwao katika hili la usalama mitandao kupitia chombo chao
kiitwacho ENISA kinacho hudumia mataifa yote yaliyo ndani muungano wa
nchi za ulaya katika maswala ya Usalama mitandao.
Tayari kume endelea kuonekana
jitihada mbali mbali zikifanyika kupitia majukwaa yetu ya kimtandao
ambapo tunajadili mambo mbali mbali na kuu limekua kukumbushia
ushirikiano huku wengi wakionekana kuelezea wazo hili la ushirikiano
nililo litoa mkutanoni limeendelea kusikilizwa na mataifa makubwa huka
mataifa mengine yakihamasishwa kuiga mfano.
Tanzania kumekua na Kauli kama
Umoja ni nguvu, Kidole kimoja hakifunji chawa, Umoja ni ushindi na
nyinginezo zinazo hamasisha ushirikiano katika nyanja mbali mbali lakini
katika hili la kuunganisha nguvu katika maswala ya uthibiti wa uhalifu
mtandao bado naona safari ni ndefu.
Nalisema hili kwa sababu bado
uhalifu mtandao unaendelea kukua na ki uhalisia vitengo vinavyo husika
na hili nchini bado vimekua havionekani kuungana na kua na uwezo mmoja
madhubuti kwa kuhimili uhalifu huu. Kuungana ninaotegemea mimi ni pamoja
na kushirikiana katika taarifa, Vitendea kazi pamoja na wataalam ambapo
kwa ujumla wake yote matatu yame gawanywa inayopelekea kuto onyesha
matunda tegemewa.
Nitatolea mfano uhalifu mpya
uliokuja kwa kasi nchini na wengi wamonekana kuathirika huku athari ya
uhalifu huu baada ya kujaribu kujadiliana na wngine wameweza kueleza
athari kubwa ipo kwa Tanzania na isipo angaziwa baadae inaweza kuibua
uhalifu mwingine ambao utakua ni matunda ya huu ulioko sasa na pengine
kua na madhara makubwa sana kwa taifa kiujumla.
Nitoe wito katika hili kwa
watumiaji wa mitandao ya kijamii kufahamu ya kua hawana buni kuhakiki
wanaendelea kua na tabia ya kujijengea ulinzi katika ngazi ya mtu
binafsi mtandaoni huku wakiwa makini sana na kutafakari sana kabla ya
kuandika “THINK BEFORE YOU INK” huku umakini na kubadilisha maneno ya
siri kua ni moja ya tabia ya watumiaji mitandao kwani neno la siri
madhubuti na linalo badilishwa itakikanapo husaidia kuzuia uhalifu wa
udukuzi.
Matumizi salama ya mitandao ya
kijamii na kutambua utumiapo mtandao wa kijamii kusemea wengine vibaya
au kutumia lugha zisizo rafiki kwa wengine inasababisha uhalifu aina ya
Cyberbulling ambao umeendelea kugharimu sana uhai wa watu duniani
kote.kuendelea kuangaza macho kwenye mifumo yetu yote ya digitali pia ni
muhimu sana kwani ukuaji wa matumizi ya digitali katika maisha yetu
lazima tujue yanakuja na changamoto za ukuaji wa uhalifu mtandao hivyo
hatuna budi kuongeza umakini katika usalama mitandao.
Faragha zetu katika mitandao ya
Kijamii nazo ni zakuangaliwa sana kwani baadhi ya malalamiko ya kihalifu
mitandao inatokana na faragha kua na mapungufu ambapo inatoa fursa kwa
wahalifu mtandao kupata taarifa za watu binafsi mitandaoni kirahisi
sana. Hili linapelekea wengine kutumia mapungufu hayo kutengeneza
mitandao ya kijamii feki yenye taarifa za watu wengine na picha zao
walizo zipata kupitia mitandao ya kijamii iliyo wazi (faragha dhaifu).


0 comments :
Post a Comment