Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limegundua kwamba kuna baadhi ya
wagombea wa vyama vya siasa ambao wameanziasha mtindo wa kutembelea
maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kama vile vituo vya daladala,
masoko mbalimbali, n.k. kwa madai ya kuyatembelea makundi ya watu wenye
kipato cha hali ya chini.
Kutokana
na uzoefu uliojitokeza katika ziara hizo zisizo rasmi ni kwamba
imeonekana mikusanyiko mikubwa isiyotegemewa katika hali ambayo
inaashiria uvunjivu wa amani. Wakati wa ziara za aina hiyo yamejitokeza
makundi ya watu mbalimbali kama vile waendesha bodaboda, machinga na
makundi mengine katika namna ambayo imeleta taharuki pamoja na usumbufu
unaotokana na makele, msongamano au shughuli za usafiri kusimama kabisa.
Tarehe
25/08/2015 majira ya saa 12:00 mchana katika makutano ya mtaa wa SWAHILI
na UHURU Kamnda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Kamishna Msaidizi
Mwandamizi LUCAS MKONDYA alilazimika kukutana ana kwa ana na mgombea
urais wa CHADEMA Mhe. EDWARD LOWASA ili kumpa tahadhali hiyo ya
kiusalama. Mgombea huyo alikuwa amezungukwa na wapanda pikipiki
wasiopungua arobaini pamoja na magari mengi katika hali ambayo ilileta
msongamano katika eneo hilo ya barabara za Swahili na Uhuru. Msongamano
huo ulileta athari na malalamiko kutoka kwa watumiaji wengine wa
barabara jijini Dar es Salaam.
Aidha,
imegundulika kwamba mgombea huyo alianzia kuzunguka maeneo mbalimbali ya
Temeke kuanzia tarehe 24/08/2015 akitumia vyombo mbalibali vya usafiri
ikiwemo mabasi ya abiria.(VICTOR)
Ni lazima
ieleweke wazi kwamba moja ya kazi za Jeshi la Polisi ni kuthibiti
makundi makubwa ya watu katika namna ambayo kiongozi yeyote wa aina ya
wagombea urais anatakiwa kulindwa katika kipindi chote cha kampeni hadi
siku ya uchaguzi n.k. Ni vyema wagombea mbalimbali hususani wagombea
urais waonyeshe ushirikiano wa hali ya juu kwa Jeshi la Polisi ili
kuzuia madhara ya aina yoyote dhidi yao. Hivyo, ni muhimu wakajihadhari
kwenda katika makundi yasiyo rasmi kwa sababu za kiusalama.
Tunawashauri
viongozi wa vyama pamoja na wagombea wao wafuate ratiba za kampeni za
mgombea urais/mgombea mwenza kwa vyama vya siasa kama ilivyotolewa na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuondoa hisia za kufanyika kampeni nje ya
ratiba.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
DAR ES SALAAM
0 comments :
Post a Comment