- Written @nkupamah blog
Wagombea
ubunge wa majimbo ya Kawe na Ubungo kwa tiketi ya Chadema, wamedai
kubaini kadi 100 za wapigakura ambazo hazina taarifa.
Walidai
jana kuwa kadi hizo ni mpango wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),
kujiandaa kuisaidia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Hata
hivyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Kailima Kombwey alisema hafahamu
kuhusu kadi hizo, huku akishauri suala hilo lipelekwe polisi ili
waliohusika wakamatwe.
Akizungumzia
madai hayo katika mkutano na wanahabari, mgombea wa Ubungo, Saed
Kubenea alidai, “Hapa tunazo 100, lakini tume imeandaa kadi kati ya
2,000 hadi 3,000 ambazo zitatumika kuwaandikisha wapigakura wengine kwa
lengo la kuisaidia CCM.”
Aliwaonyesha waandishi wa habari kadi hizo, kisha kuziwasilisha kwa Wakili, Frederick Kihwele aliyekuwapo katika mkutano huo.
Mgombea
wa Kawe, Halima Mdee alisema uhakiki katika daftari la mpigakura
unatakiwa kufanyika katika vituo vya kuandikisha kura badala ya kwenye
ofisi za kata.
Alisema kata yenye watu 70,000, wananchi wake hawawezi kufanya uhakiki kwa siku nne zilizotolewa na NEC.
Mdee alidai kuwa wamepata taarifa kuwa wakimbizi 70,000 wameandikishwa kwa siri kwenye daftari hilo mkoani Kigoma.
Hata
hivyo, Kombwey alisema hakuna mkimbizi aliyeandikishwa. Akizungumzia
siku za uhakiki katika daftari la mpigakura, Kombwey alisema suala hilo
ni la kisheria na tume haiwezi kupingana nalo..
0 comments :
Post a Comment