Mshindi wa TMT 2015 #mpakakieleweke, Denis Laswai akiwa ameinua mikono juu kuashiria ishara ya kumshukuru Mungu Mara baada ya Kutangazwa Mshindi wa TMT 2015 #mpakakieleweke msimu wa pili katika fainali iliyofanyika usiku wa kumkia leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar Es Salaam.
Mshindi
wa shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 #mpakakieleweke Denis
Laswai kutoka Kanda ya Kaskazini Arusha akiruka juu kwa furaha mara
baada ya kutangazwa Mshindi wa Kitita cha Shilingi Milioni 50 za
kitanzania mara baada ya kuibuka kinara kwenye fainali hiyo ya TMT
iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,
Jijini Dar Es Salaam.
Majaji wa Shindano la TMT wakifuatilia matukio yanayoendelea katika fainali ya shindano la TMT 2015 linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho huku ikirushwa live kupitia Live na Kituo cha ITV
Mshindi
wa TMT #reachforthestars msimu wa Kwanza Mwanaafa Mwinzago akifurahia
jambo mara baada ya Mshindi wa TMT msimu wa pili kutangazwa katika
fainali ya TMT iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa.
Walimu
wa washiriki wa TMT 2015 #mpakakieleweke Mwl Issa (Kushoto) akiwa na
Mwalimu wenzake Dkt Mona Mwakalinga wakifuatilia shindano la TMT
Mtangazaji
wa Radio One/ITV Rehema Nyamaka (kulia) akiwa na shostito wake
wakifuatilia shindano hilo lililokuwa likirushwa live na kituo cha
Runinga cha ITV usiku wa Kumakia leo
Meneja
Mradi wa TMT Saul Mpock (Kushoto) akimpongeza Mshindi wa TMT 2015
#mpakakieleweke Denis Laswai (Katikati) huku akipongezwa pia na Bi
Jennifer Kway, Mhasibu wa Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ndio
waandaaji wa shindano la TMT kwa Msimu wa Pili Sasa.
Baadhi ya
wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu, wadau kutoka Basata na
washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya ishirini bora wakifuatilia
fainali hiyo.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza (Kulia) akimpongeza mshindi wa
TMT 2015, Denis Laswai mara baada ya kutangazwa kuwa kinara wa TMT 2015
#mpakakieleweke
Haji Mboto kazini
Ruby
akitoa burudani wakati wa fainali hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo
na kupelekea Denis Laswai kutoka Mkoani Arusha Kuibuka Mshindi wa TMT
2015 #mapakkieleweke
Watu mbalimbali wakifuatilia fainali ya TMT katika ukumbi wa makumbusho ya taifa usiku wa kumakia leo
Washiriki
wa TMT 2015 #mpakakieleweke waliofanikiwa kuingia hatua ya kumi bora
wakiwa mbele ya majaji na watazamaji wa fainali hiyo iliyokuwa ikirushwa
live kupitia ITV.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Na Josephat Lukaza – Lukaza Blog
Shindano
la TMT hatimaye limefikia mwisho usiku wa kumkia leo katika Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa mara baada ya Kijana Denis Laswai kutoka Kanda ya
Kaskazini Mkoani Arusha Kuibuka kidedea kwa kuwagaragaza Washiriki
wenzie tisa waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali na kuondoka na Kitita
cha Shilingi Milioni Hamsini za Kitanzania huku washiriki tisa kuondoka
na kifuta jasho mara baada ya shindano hilo kumalizika.
Shindano
la TMT limechukua takribani miezi minne tangua kuanza kwa Mwaka 2015
huku likiwa limetembelea kanda sita za Tanzania na ha hatimaye kupata
washindi wapatao 20 kutoka katika kanda hizo ambao waliingia katika
mjengo wa TMT na kuanza kupatiwa mafunzo ya sanaa na walimu wa Chuo
Kikuu cha Dar Es Salaam
Mara
baada ya washindi hao kupatikana na kuingia ndani ya mjengo wa tmt
washiriki kumi waliweza kuaga mashindano hayo katika hatua ya mchujo na
kubakiwa na washiriki wengine kumi ambao ndio waliofanikiwa kuingia
hatua ya fainali.
Mara
baada ya mshindi wa TMT 2015 #mpakakieleweke kupatika hapo usiku wa
kumkia leo washiriki hao kumi watatengeneza filamu ya pamoja huku
wakinufaika na filamu hiyo kuanzia utengenezaji wake hadi kuuzwa .
Mshindi
wa TMT 2015 #mpakakielewe ni mshindi wa msimu wa pili wa shindano hili
lililofanyika takribani kwa mwaka wa pili sasa huku Mshiriki wa kwanza
kabisa akiwa ni Binti mdogo kutoka Kanda ya Kusini Mkoani Mtwara
Mwanaafa Mwinzago ambae mara baada ya kushinda alipata nafasi ya
kusomeshwa na kampuni ya Proin Promotions Ltd bila zawadi yake kuguswa.
Washiriki kumi bora watakuwa chini ya mkataba wa kampuni ya Proin
Promotions Ltd ambao ndio waratibu na waendeshaji wa shindano hili kubwa
Afrika Mashariki na Kati huku shindano hili likiwa limepigwa tafu na
Paisha, Pepsi, Camgas, Precision Air, Global Publishers, Data Vision
International, I-View Studio, Van Maria Boutique, Hartman Barber Shop,
na Hussein Pamba Kali
0 comments :
Post a Comment