@nkupamah blog
Na Mark B. Childress, Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mwaka
mmoja uliopita wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani,
niliandika makala kuhusu jitihada za kuwa na kizazi kisicho na UKIMWI
nchini Tanzania. Toka wakati huo, kwa pamoja tumepiga hatua muhimu
kuelekea katika kufikia azma hiyo, tukielekeza rasilimali na shughuli
zetu kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi nchini kote. Hata hivyo, bado
tunahitajika kuongeza nguvu na kufanya zaidi. Bila ya kuongeza kasi yetu
katika mwelekeo huu, maambukizi mapya yataongezeka, jambo
litakaloongeza idadi ya Watanzania watakaokuwa wakiishi na VVU hivyo
kuathiri maendeleo na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Kipindi
cha miaka mitano ijayo ni kipindi muhimu sana katika kufikia lengo la
kutokomeza kabisa UKIMWI duniani ifikapo mwaka 2030. Rais Obama ameweka
malengo makubwa kwa Mpango wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI
(PEPFAR), akitangaza kuwa hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017, PEPFAR
itakuwa inawasaidia watu milioni 12.9 kupata matibabu yanayookoa maisha
ya kufubaza VVU na kuwawezesha wanaume milioni 13 duniani kote kupata
tohara. Aidha, kwa kushirikiana na wadau wa kiserikali, asasi za kiraia
na sekta binafsi, PEPFAR itajielekeza katika kupunguza maambukizi ya
VVU kwa asilimia 40 miongoni mwa wanawake vijana na wasichana katika
nchi zilizoathiriwa zaidi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments :
Post a Comment