Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi
nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally ‘Kaseja’ nyaraka za
Pikipiki Dar es Salaam jana ambayo ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa
kikosi hicho wakati wa kampeni.(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Mbunge
wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha
wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally ‘Kaseja’ kibao cha namba za
Pikipiki Dar es Salaam leo.
Zungu
amesema ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa kikosi hicho wakati wa
kampeni alipofika kituoni hapo wakati alipopita kumuombea kura aliyekuwa
mgombea Urais Dk John Pombe Mgufuli kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
ili iwasaidie kuongeza kipato.
Mbunge huyo aliendelea kusema ataendelea kusaidia maswala ya michezo ili
kuinua sekta hiyo kwa kusaidia vifaa vya michezo Zungu ameongeza na
kusema ” Leo nakusaidieni Pikipiki iwe mali ya timu si mali ya mtu,ya
wafanyabiashara wenyewe, na niliweka ahadi ya kuwawekea mahema kwenye
maeneo mnayouzia samaki, Nitatekeleza hilo kabla ya mwezi wa kumi na
mbili ili mfanye biashara kwa uhuru.
0 comments :
Post a Comment