Monday, November 30, 2015
Balozi
wa mfuko wa pensheni wa PSPF Mrisho Mpoto Maalufu kama (Mjomba) akitoa
burudani pamoja na kutoa elimu kwa wananchi waliofika kupata elimu juu
ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa Hiari kupitia
kampeni ya mtaa kwa mtaa iliyofanyika jijini Dar
Afisa
wa mfuko wa pensheni wa PSPF Hadji Hamis Jamadary akitolea ufafanuzi
kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko wa PSPF hasa katika uchangiaji wa
Hiari ambapo aliwasisitiza wananchi kuwa kila mwananchi anaweza kujiunga
na mfuko huo na kusisitiza hakuna makato yoyote anayokatwa mteja
anapojiunga na mfuko huo.
Wananchi wakendelea kufuatilia kwa makini elimu iliyokuwa ikitolewa na maafisa wa PSPF kupitia kampeini yao ya Mtaa kwa Mtaa.
Balozi
wa mfuko wa pensheni wa PSPF Mrisho Mpoto Maalufu kama (Mjomba)
akizungumzana vyombo vya habari kuhusu kampeni ya mtaa kwa mtaa
iliyofanyika jijini Dar kushoto ni Afisa wa mfuko wa pensheni wa PSPF
Hadji Hamis Jamadary.
Na Mwandishi Wetu
Mfuko
wa hifadhi za jamii wa pensheni (PSPF) kwa kuwajali watanzania
waanzisha kampeni ya mtaa kwa mtaa ili kuweza kuungana na wananchi wa
maeneo mbalimbali kwa kuwapa elimu inayohusu mfuko huo wa pesheni
kampeni hizo zimeanzia jijini Dar es salaam kwa kutembelea wilaya zote
tatu huku wakipita mitaa mbalimbali ya wilaya hizo.
Kampeni
hiyo imeanza muda mfupi tu mara baada ya mfuko wa pensheni wa PSPF
kuungana kwa kutoa huduma na Mfuko wa afya wa NHIF ambapo wanachama wote
walio jiunga na kusajiliwa na mfuko wa PSPF watapata manufaa ya
kutibiwa kupitia mfuko huo wa afya wa NHIF kutokana na kuwa wanachama
hai.
Balozi
wa mfuko wa pensheni wa PSPF Mrisho Mpoto Maalufu kama (Mjomba) pia
naye aliweza kuungana na maafisa wa PSPF kwa kwenda kutoa elimu juu ya
uchangiaji wa hiari ambao unamuhusu kila mmoja katika jamii zetu Mpoto
amesema kuwa kwa kuonesha mfuko wa PSPF hauko mbali na wala haujawatenga
wananchi uliamua kuaznisha uchangiaji wa hiari ili kuwapa fursa
watanzania na kunufaika na mifuko ya jamii hususani PSPF ambao wanamjali
na kuthamini kila mtanzania
Naye
kiongozi wa msafara katika kampeni ya mtaa kwa mtaa iliyoanza jijini
Dar es salaam Afisa wa mfuko wa pensheni wa PSPF Hadji Hamis Jamadary
amesema "Tumeweza kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya jiji ndani ya
wilaya zote tatu ambazo ni ILALA,KINONDONI na TEMEKE kwa kuwapa elimu
wananchi ya namna watakavyo weza kunufaika na mfuko huu wa jamii" ambapo
alisema wananchi wamekuwa na mwitikio mkubwa sana hasa kwakuona mfuko
wa pensheni wa PSPF umeamua kuwafuata katika maeneo yao na kuwapa elimu
hiyo ya uchangiaji wa hiari.
Pia
Afisa matekelezo wa mfuko wa pensheni wa PSPF Albert Feruzi amesema
katika kuendeleza kutekeleza majukumu waliyo pewa ni pamoja na kuwajuza
wananchi kitugani kinacho toka katika mfuko wa PSPF ambapo alisema kwa
kila mwananchi atakaye jiunga na kusajiliwa na mfuko ataweza kunufaika
na huduma mbalimbali zinazopatikana PSPF pekee na wala sio kwingine
alizitaja baaadhi ya huduma ikiwa ni pamoja na kupata mikopo mbalimbali
kwa wajasiliamali,mkopo wa nyumba zilizopo katika mikoa mbalimbali ya
Tanzania cha muhimu ni kujiunga na kuwa mwanacha uliye hai ambaye kila
wakati unakuwa na uwezo wa kuchangia kila mwezi
Aidha
naye afisa uendeshaji wa mfuko wa pensheni wa PSPF Dolphin Richard
aliweza kupata fursa ya kuongea na wananchi katika maeneo mbalimbali
huku akisisitiza suala la kuwa ni mmoja wa wanafamilia wa PSPF kutakupa
faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupata matibabu kwa bima kwakuwa
wameweza kuungana na NHIF ilikuleta maendeleo katika taifa la Tanzania
Pia
kunukuu kauli mbiu ya Rais wa Jamuhuri Ya Muungano ya Tanzania Mh.John
Pombe Magufuli akisema (PSPF HAPA KAZI TU) amabapo watahakikisha
wanakuwa bega kwa bega na wananchi ili kila mmoja awe na usawa wa maisha
naye alitaja baadhi ya mafao wanayo yatoa ambapo ni fao la kustaafu
kazi,fao la elimu,fao la uzazi.
Afisa wa mfuko wa pensheni wa PSPF Hadji Hamis Jamadary akiwagawia wananchi fomu za kujiunga na uananchama wa mfuko wa PSPF
Baadhi ya waananchi wakijaza fomu za kujiunga na mfuko wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga ambapo kila mwananchi anaweza kujiunga.
0 comments :
Post a Comment