Sunday, November 15, 2015
@nkupamah blog
Athari za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, zimeanza kujitokeza Zanzibar ambapo jumla ya wanawake wanane wamepoteza ndoa zao baada ya kulazimishwa kupiga kura kinyume na matakwa yao, kinyume na demokrasia ya mfumo wa vyama vingi.
Wakizungumza
na mtandao huu wanawake hao walidai kwamba wamepewa talaka na waume zao
ambao walikuwa wanataka pamoja na kuwalazimisha kufahamu wanakweda
kumpigia mgombea gani ambaye wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi
Oktoba ambao ulifutwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC).
Mkazi
wa Kijiji cha Kandwi, mkoa wa Kaskazini, Jimbo la uchaguzi la Nungwi
Unguja Tatu Mkombe alisema alikatazwa na mume asiende kupiga kura kwa
sababu kura yake inaweza kusababisha fitina kubwa katika nchi.
“Mimi
ni mfuasi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na mume wangu anatoka Chama cha
Wananchi (CUF), alinikataza nisiende kupiga kura kwa madai kwamba kura
yangu inaweza kusababisha fitina kubwa katika nchi hii, lakini
nilipomuuliza fitina gani alishindwa kuniambia,” alisema na kuongeza
kuwa alipinga uamuzi huo na alikwenda kupiga kura na ndipo aliporudi
alikuta tayari talaka yake imewekwa katika kabati na kukabidhiwa.
Hata
hivyo, Tatu alisema amepokea ombi la mumewe akimtaka warudiane na
kwamba na yeye amekubaliana na maamuzi hayo ingawa kwa shingo upande
zaidi kwa ajili ya kulinda matunzo ya watoto wake wanaofikia sita ambapo
katika kipindi cha wiki mbili walichotengana malezi yote yalikuwa juu
yake.
“Nimeamua
kurudi kwa mume wangu sina ujanja kwa sababu malezi yote ya watoto
katika kipindi cha wiki mbili yameniangukia mimi huku mume wangu hana
habari na jambo lolote,” alisema.
Salma
Ibrahim Sultani (40), mkazi wa Kivunge alisema talaka aliyopewa sasa ni
ya pili ambapo awali alipewa katika kipindi cha uandikishaji wa daftari
la kudumu la wapiga kura na mumewe kwa kumshutumu kuleta ndugu zake
kuandikishwa katika jimbo la Mkwajuni ili kuiunga mkono CCM.
Alisema
mara baada ya kupewa talaka ya pili amechukua uamuzi na kusema kamwe
hawezi kurudi tena katika ndoa yake hiyo kwani hawezi kuishi kwa
shinikizo la kisiasa.
Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) Zanzibar, Mzuri Issa alikiri kupokea taarifa hizo zinazohusu matukio ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake dhidi ya waume zao, ikiwemo utoaji wa talaka kutokana na tofauti za kisiasa.
Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) Zanzibar, Mzuri Issa alikiri kupokea taarifa hizo zinazohusu matukio ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake dhidi ya waume zao, ikiwemo utoaji wa talaka kutokana na tofauti za kisiasa.
Akifafanua
zaidi Mzuri alisema Tamwa kupitia watendaji wake wameanza kulifanyia
kazi suala hilo kwa kina kufahamu ukweli wake ukoje.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais, Mama Asha Suleiman ameeleza kusikitishwa na tabia hiyo iliyofanywa na baadhi ya wanaume ambao wamesahau ubinadamu na kuweka mbele tofauti za itikadi za kisiasa.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais, Mama Asha Suleiman ameeleza kusikitishwa na tabia hiyo iliyofanywa na baadhi ya wanaume ambao wamesahau ubinadamu na kuweka mbele tofauti za itikadi za kisiasa.
0 comments :
Post a Comment