Kumekuwa
na sheria na kanuni mbalimbali zinazoundwa, ingawa wakati mwingine
hushindwa kutekelezeka kwa wakati. Ukifika katika hoteli ya Golden Tulip
utakuta jinsi eneo hilo linavyozidi kujengwa na kuendelezwa kama
lilivyokutwa na mpiga picha wetu. Kujengwa kwa eneo hili lililokuwa
pembezoni mwa Bahari ya Hindi ni kinyume cha sheria ya Hifadhi ya
Bahari. Tumeshuhudia maeneo mengi yakivunjwa kwa nyumba zao baada ya
kubainika yamejengwa katika hifadhi ya bahari. Haijafahamikaa mara moja
kama eneo hili limeruhusiwa kuendelezwa, ikiwa ni tofauti na jengo la
Hoteli ya Golden Tulip

Sheria
za Hifadhi ya bahari inasema ni marufuku kujenga nyumba mita 60
ilipokuwa bahari. Hali hii imeonekana kuwa tofauti baada ya kukuta
hifadhi hii ikionekana kuanza kujengwa na kuanza kuzua maswali mengi kwa
wadau wa maendeleo na Waanzania kwa ujumla wanaofuatilia mambo ya
maliasili na utalii. Kibao hiki kinaonyesha jinsi eneo hilo
lilivyotengwa kwa ajili ya kujenga jambo ambalo ni kinyume cha sheria za
mita 60 za bahari.
Gari
likipita katika barabara inayoelekea katika barabara ya Golden Tulip
Hoteli, ambayo pia inaonekana eneo hilo lililowekwa mabati kwa ajili ya
kuanza kulijenga kama lilivyokutwa na mpiga picha wetu. na chini mkazi
wa jiji la Dar es Salaam akipita katika eneo hilo, huku ikionekana
ramani mbalimbali za ujenzi huo.
0 comments :
Post a Comment