CHADEMA Waapa 'Kufa' na Profesa Sospeter Muhongo Bungeni

@nkupamah blog

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahidi kumshughulikia Bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kikidai kuwa bado hajasafishwa kwenye kashfa ya akaunti ya  Escrow.

Ahadi hiyo ilitolewa juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Handeni, akimnadi Daudi Lusewa.

Alisema baadhi ya mawaziri, akiwamo Muhongo, bado hawajasafishwa na tuhuma za rushwa zilizosababisha wajiuzulu hivyo wajiandae kwani wabunge wa chama hicho wamejiandaa kumwangusha.

Mnyika alisema amemshangaa kuona Rais John Magufuli akimteua Muhongo kwenye Wizara ile ile alikopatia kashfa, iliyosababisha Rais mstaafu Jakaya Kikwete kumtema kwenye Baraza la Mawaziri.

“Hatukubaliani na uteuzi wa Profesa Muhongo na namhakikishia bungeni patachimbika,” alisema Mnyika ambaye ni Mbunge wa Kibamba, Dar es salaam.

“Hoja yetu ya kwanza tutakapoingia bungeni tu itakuwa kushinikiza Waziri huyu ajiuzulu maana bado hajasafishwa,” alisema Mnyika.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment